Yai au Kuku nani katangulia?

Words
152
Reading
1 min
Listen
Play
10y

Hapo zamani za kale palitokea ugomvi mkubwa kati ya yai na kuku. Yai alidai kuwa yeye ndiye katangulia kuliona jua kabla ya kuku. Kuku naye alidai kuwa pasipo yeye yai asingekuwepo. Ugomvi huo ulizidi na kuwa mkubwa sana kiasi ambacho waliamua kwenda kwa mjumbe kupata suluhisho la utata huo.
Walipofika kwa mjumbe wakamweleza kile kilichowapeleka pale. Mjumbe aliwasikiliza kwa makini sana na kumpa nafasi kila mmoja kujieleza kwa namna awezavyo. Mjumbe baada ya kusikiliza pande zote mbili yaani kumsikiliza yai na pia kumsikiiza kuku ukafika wakati wa kutoa uamuzi.
Kwanza kabisa aliwaambia kila mmoja ana hoja za msingi. Kila mmoja anaishi kwa kumtegemea mwenziwe. Hivyo basi hakuna aliye bora kuliko mwenziwe. Kila mmoja ana umuhimu mkubwa sana kwa mwezake. Hivyo akawaasa ni suala jema kila mmoja wao kumheshimu mwenzake.
Fundisho tunalolipata hapa ni kwamba hata katika maisha tunayoishi leo ni vyema kuheshimiana na kupendana. Hakuna aliyebora kuliko mwingine. Kila mmoja ananafasi yake.

Yai au Kuku nani katangulia? | Ecency